0
Shirikisho la kandana nchini, TFF kupitia kamati yake ya utendaji imejipanga kuthibiti upangaji wa matokeo katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Msimu uliopita kulikuwa na malalamiko mengi kuhusiana kwa uangalifu mkubwa kuanzia msimu ujao .

TFF itatoa adhabu kali kwa mtu yoyote ambaye atapatika na hatia ya upangaji wa matokeo katika mechi, adhabu kubwa zaidi itakuwa ni kufungiwa maisha kujishughulisha na mchezo wa soka kwa yeyote ambaye atatiwa hatiani. Kumekuwa na tuhuma kwa miaka mingi kuwa kuna baadhi ya wachezaji, makocha na viongozi kuhusika na vitendo vya rushwa ili tu timu Fulani ipate matokeo mazuri.

Kuwafungia maisha wale wote watakaopatikana na hatia ya kufanya vitendo hivyo vya rushwa na upangaji matokeo itakuwa adhabu sahihi ila ni lazima watu hao washughulikiwe ipasavyo kwa kuwa mtandao wao ni mkubwa, na ufanya mambo hayo kwa siri kubwa. Msimu uliopita malalamiko yalikuwa mengi lakini hakuna aliyeshughulika nayo.


Marefa wamekuwa wakilalamikiwa sana lakini hakuna ambaye aliweza kutoa ushahidi wa moja kwa moja kwa maana hiyo jambo hilo si la TFF pekee bali ni kwa wadau wote wa soka. Waamuzi hawatakiwi kuendelea kufanya hivyo kama awali walikuwa wakifanya, wachezaji, na viongozi wenyewe. Jambo bora ni kukusanya nguvu ya pamoja ikiwezekana kuwepo na watu ‘ maalamu’ ambao watahusika na ufuatiliaji wa vitendo hivyo kwa msimu mzima.


Kamati ya mashindano ya TFF, ipo chini ya Makamu wa rais wa klabu ya Simba SC, Geofrey Nyange Kaburu, mtu ambaye yupo katika utawala wa mpira kwa kipindi kirefu hivyo anaweza kufahamu ni jinsi gani TFF wanaweza kupambana na hali hiyo. Huu ni wakati wa kunyoosha kila kitu katika soka la Tanzania na matatizo ya upangaji matokeo yamesababisha kutopatikana kwa timu bora katika michuano ya Kimataifa katika ngazi ya klabu na timu ya Taifa.


Kamati ya mashindano ya TFF iungwe mkono kuhakikisha upangaji wa matokeo na rushwa vinatoweka katika soka la Tanzania. Adhabu ya kufungiwa maisha kujihusisha na soka ni sawa kabisa, lakini katika hili watu wasitazame ‘ usoni’ na kuonea ‘ aibu’ wakati wa kufanya maamuzi kwa manufaa ya mpira. Wakati ni huu, komesha rushwa na upangaji wa matokeo katika soka la Tanzania, ili kunyanyua soka la Tanzania.


Post a Comment

AddThis

 
Top