0
Shirikisho la soka nchini, TFF limetuma maombi ya kuandaa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka 2017 baada ya nchi ya Libya kujitoa kuandaa michuano kufuatia ‘ balaa’ la vita linaloendelea katika nchi hiyo tangu kuangushwa kwa utawala wa Rais wa zamani wa nchini hiyo, marehemu, Mullar Muhammad Gaddaf mwaka 2011.
Libya ilishinda uenyeji wa kuandaa michuano ya mwaka 2013, lakini iliomba kupewa muda zaidi na nafasi hiyo ikaangukia kwa Afrika Kusini. Baada ya hali ya mambo kutotulia nchi hiyo imeshindwa kuwa tayari kwa uenyeji wa fainali za mwaka 2017.
Katibu mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema kuwa tayari shirikisho hilo limekutana na serikali kuhusu azma yake hiyo na jambo hilo linaweza kuirudisha Tanzania katika ‘ uso wa soka’. TFF ilituma rasmi maombi hayo kwa Shirikisho la soka barani Afrika, CAF. Mwesigwa alisisitiza kuwa miondombinu iliyopo inatosha kukidhi viwango vya timu mwenyeji wa fainali hizo , huku suala la usalama likiwa ni silaha ya ziada.
Wazo hilo linaweza kuwa zuri kwa sababu tayari kuna wigo mpana wa viwanja vyenye hadhi. Uwanja wa Taifa, na Ule wa Uhuru ambao upo katika ukarabati mkubwa, vinakidhi viwango vya kimataifa na vinaweza kuwa moja ya viwanja vizuri zaidi Kusini mwa bara la Afrika. CCM Kirumba, Mwanza, Sokoine, Mbeya vinaweza kukidhi viwango vya CAF na vinahitaji matengenezo madogo madogo. Pia kuna viwanja vya Amani, Zanzibar, na Gombani, Pemba labla changamoto itakuwa ni kuandaa sehemu nzuri za mazoezi kwa timu husika jambo ambalo linaweza kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.
Mara ya mwisho Tanzania ilicheza michuano hiyo mwaka 198 nchini Nigeria na haijapata tena nafasi hiyo. Mwaka 2004 nchi za Kenya na Rwanda zilifuzu kwa fainali za Tunisia kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda wamekuwa katika mapambano yenye uhai lakini hali ni mbaya kwa Stars licha ya timu hiyo kuwa katika udhamini wa kueleweka kwa miaka nane mfululizo hadi hivi sasa.
Mali walitumia nafasi ya uenyeji mwaka 2002 kutambulisha upya soka lao barani Afrika na duniani kiujumla, Equator Guinea pia ilitumia nafasi hiyo ya uenyeji miaka miwili iliyopita kufufuka kisoka na Tanzania inaweza kufuata nyayo hizo. Ni suala la muda tu kusubiri majibu na wakaguzi wa CAF, lakini nafasi ya kupewa nafasi hiyo itatufungulia njia zaidi kutangaza mpira na kuimarisha soka la Tanzania. - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=5562#sthash.NjJmsNZ2.dpuf

Shirikisho la soka nchini, TFF limetuma maombi ya kuandaa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka 2017 baada ya nchi ya Libya kujitoa kuandaa michuano kufuatia ‘ balaa’ la vita linaloendelea katika nchi hiyo tangu kuangushwa kwa utawala wa Rais wa zamani wa nchini hiyo, marehemu, Mullar Muhammad Gaddaf mwaka 2011.

Libya ilishinda uenyeji wa kuandaa michuano ya mwaka 2013, lakini iliomba kupewa muda zaidi na nafasi hiyo ikaangukia kwa Afrika Kusini. Baada ya hali ya mambo kutotulia nchi hiyo imeshindwa kuwa tayari kwa uenyeji wa fainali za mwaka 2017.

Katibu mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema kuwa tayari shirikisho hilo limekutana na serikali kuhusu azma yake hiyo na jambo hilo linaweza kuirudisha Tanzania katika ‘ uso wa soka’. TFF ilituma rasmi maombi hayo kwa Shirikisho la soka barani Afrika, CAF. Mwesigwa alisisitiza kuwa miondombinu iliyopo inatosha kukidhi viwango vya timu mwenyeji wa fainali hizo , huku suala la usalama likiwa ni silaha ya ziada.

Wazo hilo linaweza kuwa zuri kwa sababu tayari kuna wigo mpana wa viwanja vyenye hadhi. Uwanja wa Taifa, na Ule wa Uhuru ambao upo katika ukarabati mkubwa, vinakidhi viwango vya kimataifa na vinaweza kuwa moja ya viwanja vizuri zaidi Kusini mwa bara la Afrika. CCM Kirumba, Mwanza, Sokoine, Mbeya vinaweza kukidhi viwango vya CAF na vinahitaji matengenezo madogo madogo. Pia kuna viwanja vya Amani, Zanzibar, na Gombani, Pemba labla changamoto itakuwa ni kuandaa sehemu nzuri za mazoezi kwa timu husika jambo ambalo linaweza kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.

Mara ya mwisho Tanzania ilicheza michuano hiyo mwaka 198 nchini Nigeria na haijapata tena nafasi hiyo. Mwaka 2004 nchi za Kenya na Rwanda zilifuzu kwa fainali za Tunisia kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda wamekuwa katika mapambano yenye uhai lakini hali ni mbaya kwa Stars licha ya timu hiyo kuwa katika udhamini wa kueleweka kwa miaka nane mfululizo hadi hivi sasa.

Mali walitumia nafasi ya uenyeji mwaka 2002 kutambulisha upya soka lao barani Afrika na duniani kiujumla, Equator Guinea pia ilitumia nafasi hiyo ya uenyeji miaka miwili iliyopita kufufuka kisoka na Tanzania inaweza kufuata nyayo hizo. Ni suala la muda tu kusubiri majibu na wakaguzi wa CAF, lakini nafasi ya kupewa nafasi hiyo itatufungulia njia zaidi kutangaza mpira na kuimarisha soka la Tanzania.

Post a Comment

AddThis

Top