0
Martin Nooij, mkufunzi mkuu wa timu ya Taifa ya kandanda ya Tanzania, Taifa Stars, ametangaza kikosi cha wachezaji 26 ambao watachujwa na kusalia wachezaji 20 ambao watasafiri hadi nchini Morocco kucheza na ‘ Atlas Lions’ timu ya Taifa ya Morocco katika mchezo wa kimataifa wa kalenda ya FIFA, Septemba 5.

Nooij tayari ameiongoza Stars katika michezo minne ya kimashindano, akishinda mchezo mmoja dhidi ya Zimbabwe, mwezi Mei katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya kulazimisha sare jijini Harare katika mchezo wa marejeano kuwania nafasi ya kufuzu kwa FAinali za AFCON, 2015 ambazo zitafanyika nchini Morocco.

Stars itacheza na ‘ Simba wa milima ya Atlas’ katika siku ya kalenda ya FIFA, lakini wana kumbukumbu ya kuondolewa katika harakati za kufuzu kwa michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika baada ya kuondolewa na Msumbiji, wiki mbili zilizopita.. Timu hiyo itaingia kambini siku ya Jumapili hii katika hotel ya Accomodia.


Wachezaji tisa wanatoka katika klabu bingwa ya Tanzania Bara, Azam FC. Mara ya mwisho Moiocco iliifunga Stars walipokutana katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia, Juni 9, Mwaka uliopita na Stars ililazwa kwa mabao 2-1. Mbwana Samatta na Tiomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya DRC, Juma Luizio wa Zesco United ya Zambia pia wametajwa katika kikosi hicho.


Kikosi kamili ni; MAKIPA, Deogratius Munish ( Yanga SC), Mwadini Ally Mwadini ( Azam FC),
MABEKI; Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Said Mourad ( wote Azam FC), Kelvin Yondan, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Edward Charles ( wote Yanga SC), Joram Mgeveke ( Simba SC),
VIUNGO; Erasto Nyoni, Himid Mao, Salum Abubakary ( wote Azam FC), Amri Kiemba, Said Ndemla, Haruna Chanongo ( wote Simba SC), Said Juma ( Yanga SC), Mwinyi Kazimoto ( Al Markhiya, Qatar),


WASHAMBULIAJI; John Bocco, Hamis Mcha ( wote Azam FC), Mrisho Ngassa, Simon Msuva ( wote Yanga SC), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta ( wote TP Mazembe, DRC), Juma Luizio ( Zesco United, Zambia), Mwigane Yeya ( Mbeya City FC)


Post a Comment

AddThis

 
Top