Zikiwa saa chache zimepita toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi. Klabu ya Young Africans imemshitaki Emmanuel Okwi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment