Kiungo wa kimataifa wa Spain Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 5.
Alonso ambaye alijunga na Real Madrid akitokea Liverpool ametambulishwa rasmi leo hii kwenye mkutano waandishi wa habari na kutoa sababu ambayo imemfanya mpaka akaamua kuondoka Santiago Bernabeu.
Kiungo huyo ambaye juzi alitangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Hispania amesema kwamba kilichomfanya kuhama Madrid sio upinzani wa namba kama inavyodhaniwa na wengi.
“Klabu haikutaka niondoke, ulikuwa uamuzi wangu mwenyewe kuondoka. Baada ya kushinda La Decima, nilihisi nahitaji changamoto mpya. Nilihisi muda wa kuondoka umefika,” Alonso aliwaambia waandishi wa habari.
“Sikuamua kuondoka kwa sababu ya ujio wa Toni Kroos. Madrid wamefanya usajili mzuri sana na tungecheza wote kwa muda mwingi. Hivyo sikuondoka kwa sababu yake, nilihitaji tu changamoto mpya.
“Bayern ndio lilikuwa chaguo sahih kwangu mimi.” – Alonso
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment