0
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam August 28 2014 imetoa hukumu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Viwango Tanzania (TBS) Charles Ekerege kifungo cha miaka 3 jela.Ripota wa BLOG HII amesema Charles alifikishwa kizimbani akikabiliwa na makosa mawili likiwemo moja la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya dola za kimarekani 42,543 ambapo kesi hiyo ilifunguliwa Novemba 06 2013.
 Mshitakiwa alikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni; (1) Matumizi Mabaya ya Madaraka kinyume na kifungu cha sheria F 31 ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 na (2) kusababisha Hasara ya kiasi cha USD 42,543/= sawa na Tsh. 68,068,800/= kwa Shirika la Viwango Tanzania – TBS.
Ni kinyume na kanuni za adhabu – K/A 10(1) ya jedwali la kwanza ikisomwa pamoja na vifungu 57(1) na 60(2) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 kwa kusitisha ulipwaji wa 50% ya ada ya Utawala (Administrative fee) kwa kampuni za JAFFAR MOHAMED ALI GARAGE and QUALITY MOTO pamoja na kosa jingine ambalo ni matumizi mabaya ya madaraka.

Post a Comment

AddThis

 
Top