0


 Akiruka kwa furaha: Vincent Kompany akishangilia baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa EPL

KLABU ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini England baada ya kufanikiwa kuwafunga West Ham mabao 2-0 katika uwanja wa nyumbani wa Etihad.

Wanaume wa Manuel Pellegrini walijua wazi kuwa ushindi katika mechi hiyo utawapatia ubingwa wa pili ndani ya misimu mitatu bila kujali matokeo ya Liverpool dhidi ya Newcastle.

 Samir Nasri alikuwa wa kwanza kuifungia Man City bao la kuongoza katika dakika ya 6` tu ya mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani.

Bao la pili la Man City lilifungwa dakika ya 49` kupitia kwa nahodha wake Vicent Kompany na kuihakikishia  City ubingwa wa EPL.

Liverpool walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle, lakini ushindi wa Man City umewafanya washindwe kukata kiu ya kutotwaa ubingwa kwa miaka 24, sasa imefikia 25.
 Tumemaliza kazi: Vincent Kompany  akizingirwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la pili
  Vincent Kompany amewapatia ubingwa Man City



Post a Comment

AddThis

 
Top