MWENYEKITI LYAMUNDA AHIMIZA ELIMU WILAYANI BAHI MKOANI DODOMA
Mathias Lyamunda mwenyekiti wa asasi ya kiraia BANGONET wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma
Imeelezwa kuwa Wilaya ya Bahi ina changamoto kubwa ya kielimu kwa wanafunzi wanohitimu kutofanya vizuri
Hayo yameelezwa leo na Mathias Lyamunda mwenyekiti wa asasi ya kiraia BANGONET wilaya ya Bahi iliyopo Mkoani Dodoma pindi alipofika radio mwangaza fm wakati akielekea kwenye mahafali ya darasa la saba ya shule ya msingi Makanda
Bwana Lyamunda amesema kuwa,wilaya ya bahi haikufanya vizuri katika matokeo yaliyopita hasa kwa shule za sekondary ambapo kiwango cha ufaulu hakikuwa kizuri
Akifafanua viwango hivyo vya ufaulu bwana Lyamunda amsema waliyopata division 3 ni watano,division 4 zaidi ya 100 na divison 0 zaidi ya 500
Kutokana na matokeo hayo amewaasa wazazi Wilayani Bahi kuzingatia swala la elimu bila kujali jinsia ya watoto
......mwisho..........
Post a Comment