0



 Pc Athumani wa jeshi la polisi akiongea jambo na ndani ya studio za radio mwangza fm dodoma



Imeelezwa kuwa baadhi ya madereva wa magari aina zote Mkoani  Dodoma wana tabia ya kutii sheria pale tu wanapomuona askari katika eneo la ambapo wanapita 

Hayo yameelezwa leo na Pc Athumani Rashidi Muhenga wa jeshi la polisi kikosi ch ausalama barabarani Mkoa wa Dodoma  alipoongea kwenye kipindi cha moja kwa moja kinachorushwa na radio mwangza fm kila siku za jumatatu hadi ijumaa saa maoja na nusu hadi saa mbili kamili asubuhi

Amesema baadhi ya madereva wa Mkoa wa Dodoma wana tabia ya kuvunja sheria kwa kendesha gari kwa mwendo kasi,kuendeshea kushoto wakiwa kwenye barabara mbili,kufunga break ghafla au kurudsha gari nyuma akiwa barabara kuu

Pc Athumani amesema kuwa hayo ni baadhi ya makosa wanayoyafanya madereva hao lakini jeshi la polisi mkoani hapo lipo makini kuhakikisha kuwa wanawachukulia hatua wale wote ambao wanavunja sheria makusudi

..........mwisho..........

Post a Comment

AddThis

 
Top