0
Na Ojuku Abraham

BAADA ya kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’ ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo na Amani limemuibua afande wa kike baada ya kumsaka sana.
Askari aliyefukuzwa kazi kutokana na kosa la ukiukaji wa maadili, Veronica Mdeme.
Kwa mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani Kagera, askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898 Veronica Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo na kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo.
Ilidaiwa kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo Mutukura, umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao walikuwa katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazoleta umeme nchini kutoka Uganda.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.
Ilisemekana kwamba, Linga ndiye aliyewapiga picha wenzake ambao habari zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa na uhusiano wa kijamii.
Madai yalizidi kutiririshwa kwamba baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga alibaki na nakala katika kamera yake kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.
Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.
“Baada ya kuambiwa hivyo, jamaa walilegea kabisa. Mwanzoni walitia ngumu lakini walipoona jamaa amekomaa, hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye, hivyo akawa anapata kitu kidogo kila alipojisikia  na kuwa nipe nikupe na hakuna uhakika kama dada Vero alisalimika kwenye mambo mengine kwani naye alikuwa akitumia nguvu kubwa kuhakikisha mumewe hajui,” kilidai chanzo hicho.

Post a Comment

AddThis

 
Top