0


 



Mapenzi ni kitu Fulani tofauti sana kwenye hii dunia na hata nje ya hii sayari.
Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana yanasababisha hata mambo mengine kwenye hii dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na mahusiano ya mapenzi.
Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa mapenzi.

Ukiachilia mbali PESA, Mapenzi huwa yana nafasi kubwa sana kwenye kitu chochote ndani yahii dunia tunayoishi.
Si masikini wala si tajiri, wote kwa pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze kwenda sawa kwa upande wao.
Na ndio sababu hata mimi hapa ninaandika kuhusu mapenzi kwa sababu yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa sasa.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali,basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais.


Wengine hufikia hatua ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana.
Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-



           1.)UONGO( 2)USIRI WA KUPITILIZA(3) KUCHAET NA MTU MWINGINE (4DHARAU)(5)MROPOKAJI ASIYE NA SIRI (6) TAMAA?KUKOSA UVUMILIVU(7)KUKOSA MSIMAMO(8)KUTOJALI KUTOKUWA NA MSAADA(9)UBAHILI(10)USHOGA
          

 Hii sababu ya kumi ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu anayependa mtu wake awe Shoga kama ni mvulana au awe Msagaji kama ni msichana. 
Ni aibu kubwa sana kwa mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani kwa akili ya kawaida kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama utakishuhudia kwa macho yako.

Post a Comment

AddThis

 
Top