0
Kikosi cha Yanga kiliwasili salama Kisiwani Zanzibar, jana, huku kikimuacha nyota wake Danny Mrwanda jijini Dar baada ya kukosa tiketi, lakini kubwa zaidi ni kitendo cha uongozi wa timu hiyo kugomea hoteli walizoandaliwa na Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA).


Yanga ambayo ipo visiwani humo kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi ambalo limeanza jana, ililazimika kuwasambaza wachezaji wake katika hoteli mbalimbali kutokana na kukosa hoteli ya kukaa pamoja.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema wameshindwa kukaa kwenye hoteli walizoandaliwa na waandaaji wa mashindano hayo kutokuwa na hadhi kutoendana na klabu yao.

“Hoteli ambazo walitupa hazikuendana na hadhi yetu, tukaamua kutafuta wenyewe nyingine, lakini nyingi tukakuta zimejaa, nafikiri hii inatokana na shughuli ya mapinduzi inayoendelea kisiwani hapa, hivyo wachezaji wamesambaa katika hoteli tofauti huku tukiendelea kutafuta hoteli moja ya kukaa wote,” alisema Muro.


Kuhusiana na ishu ya Mrwanda, ofisa huyo alisema Kocha Hans van Der Pluijm alitaka kusafiri na wachezaji wote lakini ZFA wakatuma tiketi za wachezaji 21, hivyo Mrwanda akabaki Dar lakini anatarajiwa kujiunga na wenzake leo Ijumaa.

Post a Comment

AddThis

 
Top