0
Uongozi wa Tawi la Mpira na Maendeleo maarufu kama Simba Ukawa, umeibuka na kumtetea aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mzambia, Patrick Phiri kuwa hakuwa na tatizo klabuni hapo.


Simba iliamua kuachana na Phiri baada ya kuona mwenendo mbaya wa timu huku nafasi yake ikizibwa na Mserbia, Goran Kopunovic.

Katibu wa tawi hilo, Mohamed Ally ‘Ngumi Jiwe’ alisema kumfukuza Phiri ni kosa kwani timu ilikuwa katika hali nzuri lakini viongozi ndiyo waliokuwa wanasababisha matokeo mabaya katika  kila mechi.

“Tatizo ndani ya Simba si Phiri bali ni uongozi, unamtolea nini kocha ambaye akifanya vizuri sawa lakini akiharibu moja basi maneno mengi.

“Kama unakumbuka rais wetu Evans Aveva alisema kuwa tatizo la Simba ni wachezaji ambao ni (Amri) Kiemba na (Haruna) Chanongo lakini bado timu imeendelea kufanya vibaya,” alisema Ngumi Jiwe.

Post a Comment

AddThis

 
Top