0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Vijijini amejitolea kuisaidia timu ya Ndanda kuhakikisha inabaki Ligi Kuu Bara kwa kujitolea fedha kiasi cha shilingi milioni 4.5 na posho za wachezaji kwa wiki.


Ndanda inashikilia mkia katika msimamo wa ligi kuu kufuatia kuwa na pointi sita ikiwa imeshinda michezo miwili na kupoteza michezo sita hivyo kujikuta katika wakati mgumu.

Mbunge huyo alitoa kiasi hicho kutokana na kukabiliwa na ukata ambapo kiasi cha shilingi milioni 3 zitatumika kwa ajili ya malazi na chakula huku milioni 1.5 kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya michezo kwa wachezaji.

Msemaji wa Ndanda, Idrisa Bandari alifunguka kuwa kiasi hicho cha fedha kitasaidia timu hiyo kuwa katika kiwango kizuri ambapo waziri pia ameahidi kutoa posho ya shilingi milioni 1.2 kwa wiki hadi msimu utakapoisha.


“Hii ni changamoto kwetu kuhakikisha timu yetu inabaki katika ligi kwani hakuna anayependa kuwa katika nafasi tuliyipo sisi,” alisema Bandari.

Post a Comment

AddThis

 
Top