0
Steven Gerrard (kulia, anayekimbia na Mario Balotelli) ruksa kuongea na timu nyingine.
Liverpool wanajiamini Steven Gerrard atasaini mkataba mpya Anfield hata kama nahodha wao huyu yuko huru kuzungumza na klabu nyingine kuanzia leo siku ya kwanza ya mwaka mpya.
Gerrard ameingia kwenye miezi sita ya mwisho ya  mkataba wake na nyota huyo mwenye miaka 34 kwasasa anaweza kuzungumza na timu nje ili kujiunga nazo majira ya kiangazi mwaka huu.
Toronto FC na New York Red Bulls wote wameeleza nia ya kumsajili Gerrard ili akacheze ligi ya Marekana, MLS.
Pia
anahusishwa na kujiunga na Inter Milan.

Post a Comment

AddThis

 
Top