0
Wilfried Bony anawindwa na Manchester City 
Manchester City wameanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Swansea City, Wilfried Bony kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 25.
Mwenyekiti wa Swansea,  Huw Jenkins  alisema jana kuwa klabu yake haijapokea ofa yoyote mpaka sasa, lakini City wameshafungua mazungumzo ili kumnasa Muivory Coast huyo ambaye
pia
anawaniwa na Real Madrid.
Mazungumzo yalifanyika na washauri wa Bony jana usiku.
Wiki ijayo Bony ataenda Abu Dhabi ambapo Ivory Coast imeweka kambi ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika mwaka huu

Post a Comment

AddThis

 
Top