0
NI fununu tu! Mwanamuziki wa kizazi kipya, Juma Jux, ameweka bayana kile kinachoendelea kati yake na Vanessa Mdee ‘V Money’ kuwa ni mambo ya kikazi na si uhusiano wa kimapenzi.


Msanii wa muziki wa RnB nchini Tanzania, Jux akipozi katika studio za Global TV Online.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Global TV Online, Jux aliyasema hayo kutokana na tetesi zilizokuwa zikiandikwa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba amejiweka kwa mwanadada huyo anayetamba na Wimbo wa Siri alioshirikiana na Barnaba.
 Ni fununu tu, hakuna jingine. Mimi na Vanessa tupo kikazi, nakumbuka nilipokuwa nataka kufanya video yangu ya Sisikii, nilikuwa natafuta msichana wa kuwa naye kwenye video, kwa sababu alikuwepo, basi hakukuwa na jinsi, nikaamua kumtumia kwani aliujua wimbo vizuri hivyo nikaamini kwamba video ingekuwa poa sana na kweli ikawa hivyo,” alisema Jux.

Fununu za wawili hao kutoka kimapenzi zilianza kuvuma tangu mwishoni mwa mwaka jana ambapo walikuwa wakionekana sehemu mbalimbali wakitanua na kula bata.Kwa kutazama mahojiano zaidi kuhusu msanii huyo siku ya Jumatatu, unaweza kutembelea Global TV Online kwa kuingia www.globaltvtz.com
JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORT

Post a Comment

AddThis

 
Top