Na Musa mateja
Safari hii ndiyo basi tena! Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.
KUMBE NI MUDA MREFU TU
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa.
SAFARI YA CHINA
Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache zilizopita Wema au Madam kama anavyopenda kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda China kuchukua mzigo bila kumwambia ni mzigo gani na kwamba huko aliambatana na wanaume wanne, wawili wakiwa ni Martin Kadinda na Petit Man.
KAMA MBWAI, IWE MBWAI
Ilidaiwa kwamba wanaume wengine wawili wapo kwenye mabano, jambo ambalo Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita, hakuliafiki suala hilo lakini Madam akasema liwalo na liwe yaani kama ‘mbwai iwe mbwai’ hivyo akampuuza na kwenda zake China!
AHADI HEWA?
Chanzo hicho kilidai kwamba, kuna wakati Madam alimuomba Dangote au Chibu ampe fedha kwa ajili ya mtaji ambapo jamaa huyo alikubali lakini siku zikawa zinayoyoma bila dalili hivyo Wema akaona wa nini kama mtu mwenyewe hawezi kumsaidia?
ANAMTUMIA KIBIASHARA?
Ilisemekana kwamba, baada ya kuona hali hiyo, Wema alijiongeza na kuanza kukubaliana na makelele mengi kuwa jamaa huyo anamtumia kibiashara huku yeye akilamba shoo na kupiga fedha ndefu ndani na nje ya Bongo.
UBAHILI WAMPONZA DIAMOND
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, tabia ya Diamond ya ubahili, nayo imechangia kwa Wema kukaa pembeni kwani jamaa huyo siyo mkataji wa mkwanja kama ilivyokuwa kwa yule kigogo wa Wema, Clement.
“Wewe unamuonaje Wema? Yule mtoto bei mbaya bwana. Matunzo yake si mchezo. Sasa Dangote na ubahili wake ndiyo hivyo atamsikia Madam kwenye bomba,” kilisema chanzo hicho. nasib abdully
BMW LATAJWA
Chanzo hicho kilitiririka: “Unalikumbuka lile BMW (gari) alilodaiwa Wema kapewa na Kadinda siku ya bethidei yake? Unajua Diamond alikuwa Marekani, sasa aliporudi akataka kujua BMW imetoka wapi maana yeye alitoa Murano, hapo ndipo moto ukawaka na wakawa hawaivani tena.”
BETHIDEI YA DIAMOND
Habari ziliendelea kupeperushwa kwamba siku ya bethidei ya Diamond ambapo jamaa huyo alizawadiwa BMW X6 na uongozi wake wa Wasafi, Wema alikwenda kwenye shughuli tu ili kuonekana kwenye kamera.
Ilisemekana kwamba, ndiyo maana kwenye shughuli hiyo Diamond ndiye aliyekuwa akihaha kuhakikisha Wema hapati usumbufu tofauti na Wema aliyekuwa anafuata tu maelekezo ‘kishingo upande’ kwani ndani yake hakuna mapenzi tena.
UKIMYA WAPITA
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio lile kulipita ukimya fulani huku kila mmoja akiishi kwake tofauti na awali ambapo Diamond alikuwa akijinasibu kuwa huwa analala nyumbani kwa baby (Wema), Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.
DRAMA KWENYE BETHIDEI YA AUNTY EZEKIEL
Kwenye bethidei ya mwigizaji ambaye ni shosti wa Wema, Aunty Ezekiel, Diamond ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini kwenye Mgahawa wa Rodizio uliopo Masaki jijini Dar, huku kukiwa na taarifa kwamba Madam asingekuwepo kwa kuwa alikuwa safarini.
Wakati shughuli ikiendelea, Diamond alionekana mwenye furaha akiwa na timu yake lakini ghafla alipoibuka Wema upepo ukabadilika.
Wema alipoingia ukumbini akitokea safarini hata kabla ya kwenda nyumbani, alimpita Diamond, akaenda kusalimiana na Aunty kisha akaanza kuzunguka kwenye meza kusalimiana na mtu mmojammoja, cha ajabu alipofika upande aliokuwa ameketi Diamond na timu yake, aliwaruka na kwenda moja kwa moja kusalimiana na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe.
MINONG’ONO KILA KONA
Ishu hiyo iliibua minong’ono kila kona ya ukumbi huo na kuthibitisha zile tetesi kwamba hawapo kwenye uhusiano mzuri.Wakati Wema akifanya yake na Aunty, Diamond alipishana naye kama hawajuani na kukimbilia kwenye gari akiwa na timu yake tayari kwa kutimua.
‘HUYU DEMU SIYO’
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kwa nini Diamond na ‘kruu’ yake waliacha sherehe wakitaka kutimua, mmoja wa memba wa timu yake ya Wasafi alisikika akisema ‘huyu demu siyo, hata ungekuwa wewe ingekuuma. Jambo alilomtendea mshikaji siyo poa kabisa’.
WEMA VIPI?
Alipododoswa Wema juu ya kuzama kwake ukumbini na kumfanya Diamond achomoke bila ya kusalimiana alishindwa kutoa majibu ya kina na kusema hakujua nini kilimkimbiza ila yeye alikuwa pale kwa ajili bethidei ya Aunt na si kingine.
DIAMOND ANASEMA?
Alipofuatwa Diamond kuzungumzia juu ya kutoka nduki baada ya Wema kuingia ukumbini hapo, aliomba mwandishi wetu amwache kwa maana kwamba ampotezee na kuzama kwenye ndinga lake na kuondoka kwa mbwembwe.
Hata kesho yake alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi ili aweze kuzungumzia hilo hakuonesha ushirikiano kwani simu yake ya kiganjani haikupokelewa muda wote alipopigiwa.
TUMETOKA MBALI
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha.
Wawili hao waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kisha kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ huku cha Wema kikiwa kwa yule kigogo wake, Clement.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment