0




Nimeambatanisha na Post hii WIMBO WAKE ” AMEN ” ambao ndio utunzi wake wa Kwanza akiwa na KOFFI OLOMIDE kwenye ALBUM MAGIE.

Taarifa tulizo zipokea tokea Usiku wa kuamkia leo Tarehe 08-10-2014, Bado tulikua tukiifanyia kazi kabla yakuiweka kiwanjani, zaashiria kwamba Msanii Mwanamuziki wa Zamani wa Group Quartier Latin International BABIA NDONGA SHOKORO  kafariki Dunia JIJINI LUANDA ( ANGOLA ),kutokana na MUSHTUKO WA MOYO.

Wengi Wanaambatanisha Kifo chake na kitendo cha JB MPIANA , FALLY IPUPA, FELIX WAZEKWA, kumfungulia mashitaka DADA YAKE CHRISTINE maarufu kwa jina la ” VIEUX KISI NDJORA ” ambae tokea Jana yuku kizimbani kwenye Jela kuu JIJINI KINSHASA ya MAKALA.

Kwa utafiti wetu, yaonyeshakua, BABIA NDONGA, Tayari alikua na Matatizo ya Kifamilia katiyake na Mkewe, Usiku wa Kifo chake, Walitokea kua namabishano makali sana Namkewe, kutokana na hali hiyo, BABIA NDONGA akatondoka chini, Wakampeleka kwa Haraka kwenye Hospitali Kuu ya PREDA JIJINI LUANDA ambako umauti ukamkuta.

BABIA NDONGA CHOKORO kajiunga na Group Quartier Latin ya KOFFI OLOMIDE tokea Mwaka 1993, Album yake ya kwanza aliochangia ni ” MAGIE ” Iliotolewa Mwaka 1994.

BABIA NDONGA Kajiondoa kwenye Group hilo Mwaka 2001, Kisha akaja tena kujiunga kwa Mara Nyingine tena na Quartier Latin Mwaka 2003 nakaja kuamua kujiondoa  Moja kwa Moja Mwaka 2011.
Baada yakujiengua kwenye Group Quartier Latin, BABIA NDONGA CHOKORO kahamia INCHINI ANGOLA JIJINI LUANDA ambako kaweka Maskani yake.

BABIA NDONGA alikua kwenye Matayarisho ya Album yake ” VRAI MOMENT ” Ukosefu wa Producer wa Uhakika Album hiyo hadi leo haijafaanikiwa kutolewa.
Salamu zetu za Rambi rambi ziwaendee Familia yake, Tulimpenda sana ila Mwenyezi Mungu kampenda zaidi.

Post a Comment

AddThis

 
Top