Mwamuzi wa mchezo wa masumbwi Mageja Dziurgota amepelekwa hospitalini huko Croatia kupata matibabu baada ya kujikuta akishushiwa makonde ya kutosha na bondia Vido Loncar (18) aliyekuwa akipambana na bondia kutoka Lithuania, Algirdas Baniulis.
Janga hilo la mwaka limemkuta mwamuzi huyo mara baada ya kumtangaza Baniulis kuwa mshindi katika pambano hilo.
Shirikisho la mchezo wa masumbwi limemfungia bondia huyo kucheza pambano lolote, japo wanaamini kuwa bondia huyo si ‘mnyama’ kama anavyodhaniwa na watu baada ya kumtwanga makonde mwamuzi huyo.
Video iliyopo katika mtandao wa Youtube inayoonesha tukio zima la mkasa huo, imepata watazamaji zaidi ya milioni 2 ndani ya masaa 40, kwako mtu wa nguvu nafasi yako kuitazama pia.
Post a Comment