0
Kauli ya rapper Andre 3000 iliyochukuliwa kama sifa kubwa kwa msanii Future pale Andre aliposema Future ni msanii mwenye akili na uwezo mkubwa sana na dunia isimchukulie poa tu. Vibe 3 imeripoti kuwa Andre amesema anauwezo mkubwa ila anachukuliwa poa kwa sababu anafanya muziki wa trap.

Andre anasema alipata nafasi ya kukaa na Future na aligundua jamaa ameweza kurekodi nyimbo tatu bora ndani ya usiku mmoja au saa chache tu. Nyimbo hizi ni  Tony Montana,Racks na Turn Off The Lights.
Inasemekana Andre atamshirikisha Future’ kwenye album yake mpya baada ya Future kumshirikisha kwenye wimbo wake ‘Benz Friendz’.

Post a Comment

AddThis

 
Top