0
Beki Gerard Pique wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, amewatolea lugha kali Polisi wa Usalama Barabarani baada ya kumlamba faini ndugu yake.

Pique alifanya hivyo wakati akirejea Hispania baada ya kuitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano ya kimataifa.
Ndugu yake aitwaye Marc ndiye alipaki gari kwa dakika 15 katika eneo la mabasi na kusababisha usumbufu.
Pique ambaye ni mzazi mwenza wa mwanamuziki maarufu, Shakila alipinga hilo na kuanza kuwasukumbia maneno makali polisi hao.

“Mnanipiga faini bila sababu, au kwa kuwa mnaniona mimi ni maarufu.
“Mnafanya hivyo kusudi mpate fedha za pongezi, ngoja, nitazungumza na mabosi wenu, nyie ni dhuluma tu,” alisema akionyesha kuwa na jazba.

Hata hivyo, baadaye, Pique alilazimika kuomba radhi kutokana na kitendo hicho.

Post a Comment

AddThis

 
Top