0
BALOTELLI AKIWA NA MPENZI WAKE, FANNY NAGUESHA.
Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli amefunguka na kusema sasa amekua, wasimlinganishe na ilivyokuwa awali.

Balotelli raia wa Italia mwenye asili ya Ghana amesema wanaodhani hufanya tendo la ndoa siku ya mechi, wanajichekesha wenyewe.
Mshambuliaji huyo mwenye vituko amesema hawezi kufanya tendo la mapenzi wakati anajua ana mechi.
“Kila mtu amefanya makosa katika wakati anajua, mimi pia nimekua hivyo. Lakini usifikiri leo nitafanya mapenzi saa tatu kabla ya mechi.
“Nimekua, kuna makosa ninayajutia lakini tatizo England vyombo vya habari vinaandika mabaya ya Balotelli tu.
“Hazijali, zinaniona kama tatizo na inawezekana watu wananiona tatizo kwa kuwa vyombo vya habari vinaripoti hivyo.
“Wako hadi wanaosahau kuhusiana na mpira wangu na wanaamini mimi ni tatizo kwa kuwa vyombo vya habari ndivyo vinaripoti hivyo.

“Wanachotakiwa kujua sasa nimekua, ninakwenda ninabadilika na sitakuwa yule wa awali,” alisema Balotelli.

Post a Comment

AddThis

 
Top