0



Mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Mzee Steven Mguto amesema kuwa mahusiano yao na mdhamini wao wa zamani Kampuni ya Bin Slum Tyres hawawezi kufikia ‘ ubaya’ wa kumpeleka mahakani na badala yake amesema kuna haja ya pande zote hizo kukutana na kukaa meza moja ili kujua tatizo na kufikia muafaka.

Yafuatayo ni mahojiano ambayo mwenyekiti huyo alifanya na www.shaffihdaud.com
“ Tulikaa kamati yote ya utendaji ya klabu, na baadhi ya wajumbe waliona ni suala la hujuma hivyo walisema tunaweza kwamba ni suala la hujuma na tunaweza kuwa na kesi katika hilo”
Kuna baadhi ya mashabiki wa timu ya Coastal walikamatwa na kufikishwa Polisi kwa madai ya kuhusika na usambazaji wa Jezi zenye maandishi ya ‘ Sound’. Kipi unaweza kusema kuhusu tukio hilo ukiwa kama Mwenyekiti wa klabu?

“ Nililaumiwa sana, lakini kama mwenyekiti nilkwenda kituo cha Polisi kuwaona baada ya kupewa taarifa kuwa kuna baadhi ya wapenzi, mashabiki walikuwa wamekamatwa. Nilishtuka nilipoambiwa kuwa wapo pia hadi wanachama wa klabu. NIlikutana na mkuu wa kituo akanieleza sababu za watu hao kukamatwa, name nikamueleza yale ambayo nilikuwa nayo lakini akasema suala hilo atalishughulikia vile anavyoona yeye”

Kitu gani kiliendelea?
“ Siku ya Jumatatu tulipokwenda Polisi tuliambiwa kwamba kuna kesi ya madai. Na tumuone wakili wetu ili aweze kulishughulikia suala hilo. Labda nikwambie, mimi binafsi sioni kama tuna kesi, lakini baadhi ya wajumbe wenzangu wanaona ni kama kuna kesi. Wasiwasi wangu ni kwamba kuna vitu vingi ambavyo vinajitokeza ambavyo ukiviangalia huwezi kama kuna kesi ya msingi kwa kuwa sisi wenyewe kama Coastal Union tulishakosea wakati uliopita.

Msimamo wenu ni upi kuhusu suala hilo la kuipeleka mahakamani kampuni ya Bin Slum Tyres?
Bin Slum ni mwanachama wetu, tulikuwa na mkataba naye kama mdhamini hivyo suala la kwenda mahakamani sioni kama zuri. Tunaweza kukaa mezani ili busara itendeke. Tutakapokaa katika meza moja tunaeza kugundua makosa yalipo, na ikionekana kuna mtu amekosea ‘ aombe samahani’ na mambo hayo yaishe. Siungi mkono suala la kumpeleka mahakani mtu ambaye alikuwa na msaada mkubwa katika timu kwa muda mrefu, inakuwaje hivi sasa Bin Slum aonekane mtu asiye na msaada?”

Wewe kama mwenyekiti wa klabu unafikiri tatizo lipo wapi na nini sababu ya uwepo wake?
“ Unajua unapozungumzia ukweli kuna watu wengine wanakuona ‘ wewe’ kama upo upande mwingine ambao wao hawakubaliani nao. Hilo ni kosa, upande wangu kama mwenyekiti ni lazima niangalie ni hasara gani ambayo Coastal wataipata wakiingia katika kesi ya namna hiyo. Baadhi ya wajumbe wanaona ni lazima waingie katika kesi, jambo ambalo kwa upande wangu kama mwenyekiti wa klabu sikualiani nalo.

Wakati mnajadili hilo, Je mlitazama hilo endapo wadhamini mlio nao sasa mkataba wao utakapokwisha na kuja wadhamini wengine. Je mtawakataza mashabiki wenu kuvaa jezi za mdhamini aliyepita, wakati tunaona barani Ulaya wadhamini wakibadilika na mashabiki wanaendelea kuvaa jezi za mdhamini aliyepita.
“ Nikwambie kitu kimoja, bado sijauona mkataba wetu mpya, ingawaje naambiwa kuwa tayari upon a umeshasainiwa, tunamsubiri muhusika atakaporudi tutautazama. Unajua mdhamini wa sasa ametusaidia kwa kiasi kikubwa, hivyo ni lazima tutazame kwa umakini mkataba huo ili yasije kutokea haya ambayo yamekuwa yakileta mgongano kati ya Coastal na Bin Slum. Hili la mkataba sitalisema zaidi kwa kuwa tayari nimethibitishiwa kuwa umeshasainiwa na mkataa huo upo. Muhusika aliyesaini mkataba huu wa sasa yupo safarini atakaporudi atatukabidhi’

Post a Comment

AddThis

 
Top