Mshambulizi wa England, Wayne Rooney anahitaji kufunga bao moja tu ili kufikia rekodi ya ufungaji mabao ‘ wa muda wote’ katika kikosi cha ‘ The Three Lions’. Mshambulizi wa zamani wa ‘ Simba Watatu’ Gwiji Sir Bobby Charlton alifunga mabao 49 rekodimbayo haijapata kufikiwa. Miaka lifunga moja yakumi iliyopita, Michael Owen alionekana kama mchezaji ambaye angeifikia rekodi hiyo lakini majeraha yalimfanya kuwa nyuma kwa tofauti ya mabao tisa.
Nahodha wa England, Rooney ‘ Baba Kai’ alifunga moja ya mabao matano ya England usiku wa kuamkia leo wakati England ilipochomoza na ushindi wa kishindo dhidi ya San Marino katika uwanja wa Wembley. Mlinzi wa kati, Phill Jargierka alifunga bao la kuongoza dakika ya 24 kabla ya Rooney kufun ga bao la 48 kwa England kwa mkwaju wa penalti.
Danny Welbeck alifunga bao lake la Tatu katika michezo miwili ya England mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Andros Townsend alifunga bao la nne dakika ya 72, kabla ya wageni kujifunga bao la tano kupitia kwa Alessandro Della Valle dakika tano baada ya bao la Townsend.
Post a Comment