0
Ukiwa kama mwanaume unaweza ukajiuliza maswali mengi kuhusu habari hii lakini huu ni utafiti uliofanywa na wataalamu wenye sifa za udaktari kutoka chuo cha tiba Uholanzi ambao wamewataka wanaume kuacha kuona aibu kujisaidia haja ndogo wakiwa wamechuchumaa iwapo wanaumwa maradhi ya mfumo wa mkojo,
Inaweza pia ikawa ngumu kwako kutekeleza jambo hili lakini wametoa hofu  wagonjwa kama wanataka kupona watumie njia hii ambayo ni salama na bora zaidi kwao.

Katika Gazeti la MWANANCHI limeandika kuwa utafiti huo mpya umebaini kuwa wanaume wenye matatizo katika mfumo wa mkojo na wanaopata shida wakati wa kutoa haja ndogo wanaweza kuondoa tatizo hilo kwa kujisaidia wakiwa wamechuchumaa.

Kuchuchumaa kutawasaidia wanaume wenye tatizo hilo  kutoacha mkojo kabisa  kwenye vibofu vyao na wenye maradhi ambayo kitaalamu yanajulikana kama LUTS wanaweza kuondokana na maumivu wakati wa kukojoa mara kwa mara usiku.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha tiba cha Uholanzi wamesema pia wagonjwa wenye LUTS wakijisaidia kwa kuchuchumaa wanaondoa kabisa tatizo hilo bila ya kunywa dawa.

Post a Comment

AddThis

 
Top