0
Zikiwa zimebaki takribani siku 11 kabla ya pambano la kwanza ‘Dar es Salaam Derby’  lipigwe katika uwanja wa taifa, klabu ya Simba SC leo inatarajia kuondoka nchini kuelekea nchini South Africa kwa ajili ya kuweka fiti ili kupata matokeo chanya dhidi ya watani wao jadi, Yanga.

Simba inatarajiwa kuondoka katika ardhi ya Tanzania leo saa 1 usiku kuelekea kwa Madiba ambapo watakuwa na kambi ya takribani siku 9 kabla ya kurejea nchini tayari kwa pambano la Oktoba 18.

Simba imekuwa na mfululizo wa matokeo yasiyofurahisha katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom – walianza kwa kutoka sare ya 2-2 na Coastal Union, kisha wakatoka 1-1 na Polisi Morogoro na wikiendi iliyopita wakaambulia pointi moja nyingine kutoka kwa Stand United.

Post a Comment

AddThis

 
Top