0



Sakata la mwanasheria Damas Ndumbaro kuitwa kwenye kuhojiwa kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu ya shirikisho la soka nchini kutokana na tuhuma alizotoa juu ya Kamati ya Utendaji ya TFF limechukua sura mpya leo hii.

Kwa mujibu wa vielelezo vya barua ambazo mtandao huu umezinasa, TFF iliamuandikia barua Ndumbaro mnamo tarehe 7, Oktoba, 2014 wakimtaka aende kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu tarehe 09/10/2014 akajieleze kwa kina juu ya tuhuma alizotoa wiki iliyopita wakati akipingana na agizo la TFF  kwa vilabu shiriki vya ligi kuu ya VODACOM kukatwa asilimia tano ya fedha za udhamini.

Hata hivyo kutokana na kielelezo cha barua ya Ndumbaro kwenda TFF, inaonyesha mwanasheria huyo amewaeleza TFF kwamba hatoweza kuhudhuria kwenye kikao hicho kwa sababu siku hiyo atakuwa safarini kuelekea nchini Marekani kuhudhuria utoaji wa mafunzo katika moja ya vyuo vikuu huko nchini Marekani.

Pia Ndumbaro ameeleza angependa aelezwe kiundani kosa lake ni lipi ili aweze kujiandaa kisheria kabla ya kwenda kujitetea vizuri mbele ya Kamati hiyo ya Nidhamu.
Pamoja na hayo lakini Ndumbaro ameomba apewe muda kuandaa malalamiko yake dhidi Raisi wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi.

Kutokana na udhuru aliotoa Ndumbaro ameomba shauri lake lisikilizwe mnamo mwezi November atakapokuwa amerejea nchini.

Post a Comment

AddThis

 
Top