0
Shumbu Wembadio Papa Wemba akiwa na Mkewe Marie-Rose Amazon
Lutumba Simaro, Nyoka Longo Jossart, Felix Wazekwa, Werrason, JB Mpiana na Wengineo ni miongoni mwa wanamuziki maarufu waliowaongoza watu wengine maarufu katika harusi iliyofana ya mwanamuziki Papa Wemba na Marie-Rose Amazon, minong’ono na lawama zimetanda jiji la Kinshasa kwa wapenda burudani baada ya Mwanamuziki nguli na mkongwe mwezie Koffi Olomide kutoonekana ukumbini wala kanisani bila sababu ya msingi.

Shumbu Wembadio Papa wemba alifunga ndoa na Bibie Merry Rose Amazon katika ndoa ambayo imekuwa gumzo katioka jiji zima la Kinshasa. Akijitetea kuhusu uamuzi wa kutoshiriki kwenye harusi hiyo Koffi amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hakualikwa na hakupatiwa kadi ya mualiko wa shughuli hiyo. Kwa mujibu wa waandaaji wa shughuli hiyo wanasema mualiko ulitolewa kwa wanamuziki wote na wengine wakisikika wakisema kuwa kwa ukaribu wa Koffi ambaye ameshawahi kufanya kazi na Papa Wemba hakupaswa kungoja mualiko ili aonekane kwenye shughuli hiyo.
Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa na Mtakatifu Joseph huko Matonge na baadaye kufuatiwa na tafrija katika hoteli ya Fleuve Congo Hôtel inasemwa ilikuwa ni mahala ambapo wanamuziki wengi maarufu walikutania kama Lutumba Simaro, Nyoka Longo Jossart, Felix Wazekwa, Werrason, JB Mpiana na wengine wengi, sio rahisi kuwapata magwiji hawa kwenye mkusanyiko wa kawaida labda kwenye misiba ambapo pia huwa kila mmoja anafika kwa muda wake.
Regards

Post a Comment

AddThis

 
Top