0
ARSENE WENGER ALIFANYA MAKOSA KWA KUTOSAJILI BEKI WA KATI AU KIUNGO WA UKABAJI? - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=5692#sthash.zi4tYJqj.dpuf


ARSENAL ilihitaji mshambuliaji, hakuna wasiwasi juu ya hilo. Walimsajili Danny Welbeck dakika za mwisho za dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka huu na kukifanya kikosi chao kuwa imara zaidi ya msimu uliopita.

Washika bunduki hao wa London walimuuza Thomas Vermaelen kwenda klabu ya FC Barcelona na kwa bahati mbaya hawajasajili mrithi wake.
Walimsajili beki wa kulia kutoka Southampton, Calum Chambers, lakini wamemtumia kama beki wa kati kwasababu ya majeruhi. Sio mbaya kumchezesha beki ya kati, lakini kupambana na baadhi ya washambuliaji wa kati wa kiwango cha juu waliopo timu pinzani inaweza kuzua tatizo.
Hapa hawajaziba pengo. Kwanini Arsene Wenger hakusajili beki wa kati?. Ilionekana wazi kuwa muhimu kumsajili beki wa kati mwenye uzoefu, lakini haijafanyika.
Arsenal wamekuwa katika wasiwasi kutokana na kukosa mabeki wengi wa kati. Mbaya zaidi, kwa majira yote ya kiangazi wamemfukuzia Morgan Schneiderlin bila mafanikio na kiukweli walihitaji beki asilia wa kati.
Aaron Ramsey ni mzuri kwenye boksi. Jack Wilshere anashambuliaji zaidi na Mikel Arteta sasa ana miaka 32, hivyo kasi yake imeshuka.
Arteta ni mchezeshaji mzuri, lakini amekosa kasi ya kupambana na wapinzani na kushindwa kushinda mipira kirahisi. Katika mechi dhidi ya timu kubwa msimu uliopita, Arsenal  alipata shida kutokana na hili.
Kwa mfano katika mechi dhidi ya Chelsea na Liverpool, Arsenal walifungwa mabao 6-0 na 5-1. Arteta alihangaishwa mno katika mechi hizi mbili.
Kusajili beki asilia wa kati mwenye nidhamu na mbinu za kimpira kungekuwa na maana kubwa kwa Arsenal.
Hili lilikuwa janga tena. Kikosi cha Arsenal kimeimarishwa kwa kuwasajili Alexis Sanchez na Welbeck kuongeza ubora wa safu ya ushambuliaji na kuwa na machaguo mengi sehemu ya mbele, lakini katika mechi kubwa msimu uliopita waliruhusu magoli mengi, lakini hawajaboresha eneo la safu ya ulinzi mpaka sasa.
Safu yao ya ulinzi itayumbishwa na timu bora pinzani zenye washambuliaji wakali. Safu ya kiungo ilihitaji kuboreshwa, hali kadhalika safu ya ulinzi ilihitaji mabeki wa kiwango cha juu.
Kama Arsenal watapambana tena kuisaka nafasi ya nne msimu huu, lawama zote itabidi aangushie kocha mkuu Arsene Wenger aliyeshindwa kusajili mpaka siku ya mwisho.

Post a Comment

AddThis

 
Top