0
Arsene Wenger alisema Abou Diaby yuko tayari kucheza tena.
KOCHA Arsene Wenger anajiamini kuwa kiungo wake matata, Abou Diaby ataisaidia Arsenal kwenye mechi ya leo usiku ya Capital One dhidi ya Southampton.

Diaby ambaye ni miongoni mwa wachezaji ambao Wenger anapendelea kuwapanga katika kikosi chake, pia ataichezea Arsenal katika mechi ya jumamosi ya ligi kuu dhidi ya Tottenham.
Nyota huyo mwenye miaka 28 alipata majeruhi tangu alipojiunga na Arsenal misimu nane aliyopita.
Aliumia vibaya kifundo chake cha mguu baada ya kuchezewa rafu na beki wa Sunderland, Dan Smith mwaka 2006 na amekuwa akitonesha jeraha hilo kwa muda mrefu.
Baada ya kusumbuliwa sana msimu uliopita, Diaby alifanyiwa upasuaji mkubwa katika kifundo chake cha mguu wa kushoto na sasa ameonekana kuimarika vizuri.
‘Wiki iliyopita Diaby alicheza dakika 90 uwanja wa Villa Park katika mechi ya vijana chini ya miaka 21. Alikuwa nasi tena  jumamosi na atacheza dhidi ya Southampton siku ya jumanne (leo),” alisema Wenger.

Post a Comment

AddThis

 
Top