0
Mchezaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza, Wayne Rooney, ameteuliwa kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza leo hii na Roy Hodgson (Kocha mkuu), kwaajili ya michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya. UEFA Euro.
Rooney anachukua mikoba hiyo baada ya Steven Gerald kustaafu kuchezea timu hiyo ya Taifa baada ya tu kutolewa katika kombe la Dunia huko Brazili.
Rooney mwenye miaka 29, amesema anajisikia faraja sana kutajwa kuwa nahodha wa timu ya Taifa.
Kocha wa Timu ya Manchester United, Van Gaal, pia alishamtaja Rooney kuwa nahodha wa klabu hiyo siku kadhaa zilizopita, Hivyo basi Rooney anapata jukumu la tatu, Katika Familia kama Captain wa Nyumba (Baba), katika Klabu yake na sasa katika timu yake ya Taifa

Post a Comment

AddThis

 
Top