Mshambuzili wa kimataifa wa Ureno na klabu bingwa ya ulaya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya msimu wa 2013-2014 katika sherehe zilizofanyika jana jijini Monaco, Ufaransa.
Nyota huyo wa Real Madrid amewapiku nyota wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi, Arjen Robben alioingia nao fainali.
Wakati Neuer alishinda taji la Bundesliga na Kombe la Dunia msimu uliopita, Robben alifunga mabao 22 kwa klabu na timu yake ya taifa msimu uliopita na Ronaldo alifunga mabao 56 na kutoa pasi 15 za mabao Real Madrid na Ureno.
Mshindi wa mwaka jana, Mfaransa Franck Ribery hakuingia fainali.
Ronaldo pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia na ushindi huu ni pigo lingine kwa mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina na Barcelona.
Ronaldo pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia na ushindi huu ni pigo lingine kwa mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina na Barcelona.
Post a Comment