Mambo yanazidi kupamba moto baada ya uongozi wa Yanga kusema ulipeleka jina la mshambuliaji Emmanuel Okwi katika majina yake ya wachezaji.Yanga imesema ilipeleka jina hilo, hivyo inashangazwa kusikia Simba imemsajili na imeamua kuongeza adhabu ya kutaka afungiwe na ile faini kutoka dola 200,000 iongezeke nyingine ya dola 500,000.Kama hiyo haitoshi, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar kwamba walituma barua ya kutaka kuvunja mkataba kwa TFF wakieleza nia yao.
“TFF haikuwa bado imejibu, Okwi akatuandikia sisi barua lakini sisi hatukiandika kwake. Ilipaswa naye apelike TFF.
“Simba pia wamefanya kosa, wanajua Okwi bado ana mkataba na Yanga, lakini wamekurupuka na kumsajili ambalo ni kosa kwa mujibu wa Fifa na Caf.
“Yanga tunajua bado suala la wachezaji wa kigeni liko wazi, dirisha halijafungwa. Ndiyo maana tulipeleka jina lake tukijua kama suala la kupunguza mchezaji mmoja litafika, tutalifanyia kazi.
“Simba na Okwi, wote wanapaswa kufungiwa kutokana na kukiuka vipengele hivi. Sisi tuliamini ni watu wa busara ambao wanakuja kuendeleza soka, lakini hizi ni vurugu ambazo hazijengi,” alisema Manji.
“Tunaamini suala letu TFF italishughulikia ndani ya siku saba, ikishindikana tukakwenda Caf, Fifa au Cas (mahakama ya soka).”
HAYA NDIYO INAYASISITIZA YANGA KWA OKWI:
1. Tokea lakini laki 2 hadi laki 5, Simba pia inawahusu, wasingekubali, wangefuata utaratibu, wamemfuata mchezaji kabla ya kuanza na timu.
2. Wataiomba TFF, ikiwezekana Okwi afungiwe kucheza moja kwa moja, pia Simba kwa kuwa wamemsajili akiwa bado na mkataba.
3. Hawajavunja mkataba, barua aliyoiandikia Yanga, ilitakiwa aindikie TFF kwa kuwa yenye haikumuandikia yeye.
4. Wametoa siku 7 kwa TFF kusikiliza na kutoa majibu ya kesi yao, la sivyo watalipeleka Caf, Fifa au Cas.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment