0
Kibarua kizito: Diego Costa aliifungia Chelsea bao la kuongoza dhidi ya timu ngumu ya Leicester.

JOSE Mourinho aliwajia juu wachezaji wake kuwa ni wavivu kufuatia kucheza vibaya kipindi cha kwanza licha ya ushindi wa mabao 2-0 waliopata jana dhidi ya  Leicester.
Chelsea walibanwa mbavu kipindi cha kwanza na timu mpya iliyopanda daraja ya  Leicester  kabla ya Mourinho kuwawashia moto wachezaji wake wakati wa mapumziko.
Mabao ya Diego Costa na Eden Hazard yalitosha kuwapa ushindi The Blues katika dimba la Stamford Bridge
Vijana kazeni: Jose Mourinho aliwajia juu wachezaji wake baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Mourinho hakafurahishwa na mwanzo wa taratibu.
Alisema: “Napenda kufanya mazoezi asubuhi, lakini wiki hii nilifanya mazoezi mchana kwasababu sio hali nzuri ya kucheza mpira, unapata uvivu”.
“Kipindi cha kwanza timu ilicheza kivivu na sikupenda kabisa.
“Lakini walijiboresha kipindi cha pili na kushinda, hiki ndicho kitu muhimu zaidi”
“Wakati wa mapumziko tuliwakalipia kidogo. Niliwaambia kuwa jinsi tunavyocheza haitoshi kushinda mchezo na walikuwa katika hatari
Shangwe: Baada ya Chelsea kufunga mabao mawili, furaha ilitawala

Post a Comment

AddThis

 
Top