0


Mshambuliaji wa England, Wayne Rooney akishangilia baada ya kufunga bao dhidi ya Uruguay katika fainali ya kombe la dunia.

“Sitasahau siku Roy Hodgson aliponifanya nipae futi 10 juu. Ilikuwa katikati ya wiki mchana nikipumzika nyumbani baada ya mazoezi. Roy alinipigia simu na kuniambia: nina habari muhimu: Nilikuwa naenda kuwa nahodha wa England”.
“Sikuweza kuamini kabisa na ninaamini hali kama hiyo itajitokeza kwa Wayne Rooney wiki hii ambapo mrithi wangu atatajwa. Kwa vile nami nahusika, ndiye mtu anayestahili kwa sasa”.
Roy ana imani kubwa na Wayne. Wakati Manchester United ikiwa katika presha msimu uliopita, wakati ule kuna tetesi nyingi kuhusu nafasi yake katika timu ya taifa, bado kocha wake alimpanga katika michezo muhimu. Ilikuwa nzuri na heshima kubwa kwake.

Wakipunga upepo: Rooney (kushoto) na Steven Gerrard wakipumzika baada ya kumaliza programu ya mazoezi mjini Algarve mwezi mei 
Nahodha: Rooney (kulia) aliiongoza Manchester United katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu dhidi ya Valencia Agosti 12 mwaka huu 


Mashetani wekundu: Rooney akishangilia baada ya kufunga bao dhidi ya Swansea kwenye mechi ya ufunguzi ya ligi kuu soka nchini England.
Labda makocha wengi wanaweza kumuondoa katika kikosi cha kwanza na kumuweka benchi, lakini Roy anajua kuwa Wayne bado ana mchango mkubwa katika kikosi chake na ataendelea kuchangia kwa miaka michache ijayo.
Kwanini nadhani Wayne ndiye chaguo la kwanza?, Kiasili ni kiongozi. Mbali na kuwa mchezaji wa kiwango cha juu, ana uwezo wa kutengeneza heshima katika kikosi, Wayne ana mapenzi ya kuliwakilisha taifa lake na hataogopa majukumu hayo

Post a Comment

AddThis

 
Top