Amekosa nafasi: Kufungwa leo kunamaanisha Carlo Ancelotti hawezi tena kuchukua ubingwa wa La Liga
MAKOSA mawili ya Sergio Ramos na Xabi Alonso yameyeyusha matumaini ya Real Madrid kushinda makombe matatu msimu huu.
Real Madrid walikuwa na uwezo kwa kubeba La Liga mbele ya wapinzani wao FC Barcelona na Atletico Madrid, lakini wameshindwa kufanya hivyo baada ya kupigwa mabao 2-0 na Celta Vigo usiku huu.
Carlo Ancelotti amechizika baada ya Real Madrid kufungwa na kujitoa rasmi katika mbio za ubingwa, huku wakisaliwa na mchezo mmoja tu.
Endapo wangeshinda, vijana hao wa Santiago Bernabeu wangepunguza pengo la pointi na kufikia pointi mbili nyuma ya vinara Atletico na pointi moja mbele ya Barcelona, lakini matokeo ya jumapili yanamaanisha matumaini yamekwisha.
“Rasmi tumekosa La Liga. Ni mashindano ya kwanza msimu huu ambayo hatuwezi kushinda na itakuwa ni uongo kama tukajipa moyo,” Alisema Ancelotti baada ya mechi.
“Tulikosa wachezaji wengi muhimu, kwahiyo haikua rahisi kujiandaa na mechi hii. Tumefungwa mabao mawili mepesi kabisa, lakini tulijaribu kurudi mchezoni baada ya pale”.
“Tunatakiwa kuangalia ya mbele, sasa tunajiandaa na mchezo wa mwisho na fainali ya UEFA”.
Real Madrid watakabiliana na Espanyo katika mchezo wa mwisho wa La Liga kabla ya kuumana na Atletico Madrid katika mchezo wa fainali wa UEFA mei 24 mwaka huu mjini Lisbon, Ureno
Post a Comment