0


ANDRES Iniesta anaamni Gerardo Martino ndiye kocha bora anayeifaa Barcelona kwasasa licha ya kuwepo tetesi kuwa ataondoka majira ya kingazi mwaka huu.

Kocha wa Celta, Luis Enrique anaripotiwa kumrithi Martino aliyerithi mikoba ya marehemu Tito Vilanova msimu uliopita.

Kutolewa hatua ya robo fainali ya UEFA, kupigwa na Real Madrid katika fainali ya Copa del Rey na kushindwa kuongoza La Liga kumemuweka kitimoto Martino, lakini Iniesta amemtetea kuwa anajua kufundisha.

“Kwa upande wangu, kocha tuliyenaye kwasasa ndiye bora,” Iniesta aliwaambia Diario Ole. “Pia nitafurahi sana kuona anakaa kwa muda mefu zaidi na kuonesha uwezo wake wote”.

“Msimu wa kwanza ni mgumu kwa kila mtu. Nimeona akiwa na nia na mipango mizuri. Siku zote anatuamini”. 

‘Wakati fulani mambo hayaendi kama unavyotaka, lakini unatakiwa kujaribu. Ulimwengu wa Barcelona ni mgumu sana, sio kwake tu, hata sisi wachezaji”.
“Tumeshindwa kufanya vizuri katika nyakati muhimu. Wakati fulani mambo yanakwend vibaya”. 

“Sio kwamba unataka hivyo, ni kwasababu wakati mwingine inatokea. Unatakiwa kufanya mabadiliko bila kujali unashinda mataji au hushindi”.
Barca watasafiri kesho kuwafuata Elche katika mchezo wa La Liga na kushinda kutawapa nguvu kubwa ya kutwaa ubingwa mbele ya wapinzani wao, Atletico Madrid.

Post a Comment

AddThis

 
Top