0


MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Edin Dzeko amesema klabu yake itajituma na kucheza kwa `asilimia 200` katika mechi mbili zilizosalia.

Sare ya 3-3 waliyoipata Liverpool jumatatu ya wiki hii, imewafanya City wawe na asilimia kubwa ya kuchukua ubingwa kama watashinda mechi ya leo usiku dhidi ya Aston Villa katika uwanja wa Etihad.

Endapo City watazoa pointi tatu watakuwa mbele kwa pointi mbili dhidi ya majogoo wa jiji wenye pointi 81.

Dzeko aliyefunga bao muhimu mwaka 2012 dhidi ya QPR na kuchangia kuipa ubingwa Man City amesisitiza kuwa wamejifunza kutokana na matokeo ya mechi za mwishoni.

“Tutajitahidi kufanya kila linalowezekana na tunadhani tayari tumeshafanya kazi kubwa,” mshambuliaji huyo amekaririwa na gazeti la The Sun.

“Baada ya kushinda Goodison jumamosi ( 3-2 dhidi ya Everton), tunaenda kucheza mechi mbili za mwisho nyumbani dhidi ya Villa na West Hall, si kwa asilimia 100, ni asilimia 200 tutajitahidi kushinda”.

“Kila kitu kipo mikononi mwetu kama miaka miwili iliyopita. Nakumbuka tuliposhinda ubingwa dhidi ya QPR, kila mtu alitegemea tungeshinda kirahisi. Ilikuwa ngumu mpaka dakika ya mwisho”.

“Nadhani tumejifunza kitu fulani. Tunajua si vizuri kuidharau timu na tunatakiwa kufanya kazi yetu vizuro”.

Dzeko ameifungia Man city mabao 14 katika mechi 29 za ligi kuu alizocheza msimu huu.

Post a Comment

AddThis

 
Top