KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka ya LMA baada ya kufanya kazi nzuri msimu huu na kuwa kocha wa kwanza wa majogoo wa jiji kutwaa tuzo hiyo.
Bosi huyo wa Liverpool amefurahia msimu wake Anfield kwa kuiongoza klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili, huku akipambana mpaka mechi ya mwisho na kupigwa bao na Manchester City waliofanikiwa kutwaa `ndoo`. Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ndiye aliyemkabidhi tuzo Rodgers mwenye miaka 41 baada ya kupigiwa kura na makocha wa ligi kuu na ligi nyingine nchini England.
Usiku wa kukumbuka: Rodgers alikabidhiwa tuzo hiyo na kocha wa England Roy Hodgson (kushoto)
Rodgers alipigwa picha akiwa na Suarez baada ya kuifanikisha Liverpool kushika nafasi ya pili
Post a Comment