0


WAKATI straika mpya wa Yanga, Emmanuel Okwi akitua nchini tayari kuitumikia timu yake mpya, Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) limesema mchezaji huyo ni halali kuichezea Yanga na ndiyo maana walikubali kutoa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).
Ofisa Mtendaji mkuu wa Fufa, Edgar Watson ameuambia mtandao huu kwamba, anachojua kama bosi wa Fufa ni kwamba ni kweli Okwi amesaini kuichezea Yanga na shirikisho lake limetuma ITC kwenda Tanzania kwa Yanga ili aweze kuichezea timu hiyo.
“Kwanza nataka kuweka wazi kwamba, Okwi alikuwa na kesi dhidi ya timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia juu ya masuala ya mkataba, Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) lilimruhusu kucheza kwenye klabu ambayo anaitaka kwa muda maalum.


Okwi alipewa kibali maalum, hivyo si kweli kuwa alikuja kucheza SC Villa ya hapa (Uganda) kama mchezaji wa mkopo, huyu alipewa kibali maalum sasa hapo kuna tofauti ya kibali maalum na mkopo,” alisema Watson.
Alisema Okwi aliruhusiwa kucheza na Fifa na ruhusa ambayo amepewa haikuwa ikimzuia kuhamishwa au kusajili kwenda klabu nyingine, hakuna mahali anapozuiliwa kusajiliwa bali kilichofanyika ni sawa na ruhusa ya kucheza.
Watson alisema kilichotokea ni kati ya Villa, mchezaji na huko alikosajiliwa ni baina yao na hakuna kinachomzuia asisajiliwe.
“Kwa mazingira yaliyopo, hakuna kipengele chochote ambacho kinamzuia mchezaji mwenye ruhusa maalum kuhamishwa hivyo tumetoa ITC na hakuna ambacho kingemzuia Okwi kwenda kule anakotaka,” alimalizia Watson.
                                              mashabiki wa yanga wakisukuma gari alilopanda Okwi
                             Okwi akitabasam baada ya kupata mapokezi makubwa
                         shabiki wa yanga akifurahi na jembe lake Okwi

Post a Comment

AddThis

 
Top