0


Kwa wacongomana neno Ngulu si geni masikioni mwao ila kwa mashabiki wa dansi nje ya congo inawezekana neno hili likawa geni masikioni mwenu.Bila kuuma maneno neno ngulu linamaanisha Nguruwe ila ni msamiati unaotumiwa kwa Wahamiaji haramu ambao wanabebwa kupelekwa Ulaya kwa kivuli cha wanamuziki.

Kwa miongo kadhaa wanamuziki wa Congo wanaongoza kwa wanamuziki wanaotoka barani Afrika kufanya maonyesho mengi Barani Ulaya na America. Kwa Vijana wa Congo ndoto zao ni kufika ama Ubelgiji au UFaransa, hii ni kutokana na historia ya nchi hii kutawaliwa na Wabelgiji na lugha wanayotumia kuwa ni Kifaransa.

Masharti ya kungia nchi za TShengeni sio rahisi lakini ni nchi ambazo zinapenda sana burdani na hasa utamaduni jambo lililofanya kwa wanamuziki na vikundi vya dini kwenda kutoa burudani huko mara nyingi, mwanya huo ndioo ulikuwa unatumiwa kuwabeba hawa Ngulu na kuwabwaga huko wakiingia kwa hati za kusafiria na vibali vya kuingia (VISA) kama wanamuziki.

Inasadikiwa kuwa kwa wastani kila Ngulu mmoja alikuwa akilipa kati ya dola 3500 USD na 5000 USD kufanikisha safri yake ya kufikishwa ulaya na inasemekana kuwa Bendi moja alikuwa ikiondoka na Ngulu 10 mpaka 15. 
“ulichotakiwa kufanya ni kufanya mazoezi ya awali ya muziki ama kupiga vyombo, kwani utasajiliwa kama mwanamuziki mpya utafanya mazoezi ambayo utayatumia kutumbuiza jukwaani ukifika Ulaya na baada ya shoo unaondoka kivyako” kilisema chanzo cha habari hii nilipokuwa nikiongea naye kubadilishana mawili matatu ya muziki huu wa Congo karibuni.

Si lazima uimbe tuu kwani wakati mwingine waliwachukua vijana na kuachana nao wakifika Airport nchi husika na hapo unaanza kutafuta maisha, kuna wengine unakuta walikuwa na ndugu au jamaa huko na hao huwapokea na kukuonyesha jinsi ya kuishi huko baada ya muda huachiwa na kuanza kutafuta kivyao.

wengi wa Vijana ambao wako Ufaransa ama Ubelgiji ambao wanaitwa Le Combatant (Bana Congo) ni matokea ya wazamiaji ambao wengine bado hawaishi kihalali na wengine wameshakamilisha masharti na sasa wanaishi kihalali lakini walikwenda Europe kwa njia za panya aliongeza mpashaji habari wangu.

Kwa wasiojua tu hawa Bana Congo ndio vijana wanaoishi huko nje (Diaspora) na wanapinga siasa za Congo za Joseph Kabange Kabila, vijana wanaotaka mageuzi kwa siasa za Congo na kupingana na yeyote anayemuunga mkono Kabila na utawala wake.

Wanamuziki wakubwa kama Papa Wemba na Felix Wazekwa wao kwa nyakati tofauti waliwahi kuhukumiwa na kufungiwa Visa za Kuingia Tshengeni kwa shutuma za biashara ya Binadamu (Ngulu), pia kashfa hiyo haiwaachi Bozi Boziana, Nyoka Longo, JB Mpiana, Werasson na hata Koffi Olomide wao pia wanasemwa kujihusisha na biashara hii ambayo kwa kiasi kikubwa imechangia utajiriri wao.

February 6 2012 Mwanamuziki Papa Wemba alihukumiwa kifungo cha miaka 15 ama kulipa faini ya Euro 20,000 kwa makosa yanayohusiana na hayo.
Kwa sasa wengi wa wanamuziki hawa wanasema kuwa kwenye hali ngumu kifedha kwani hawana show za Ulaya ambazo zilikuwa zikiwalipa pesa nyingi, wengine kwa kunyimwa Visa na wengine kutokana na mahusiano yao na Bana Congo kwa kuwa walimuunga mkono Rais Kabila.

Takribani wanamuziki wote wenye majina makubwa walishiriki kwa namna moja ama nyingine kumpigia kampeni Rais Kabila ambaye alishinda na kurejea madarakani jambo lililopingwa vikali na Bana Congo na leo hii wanalipa gharama za usaidizi wao.


Post a Comment

AddThis

 
Top