0





 CoploMarini kushoto na Sajenti Kitundu ndani ya radio mwangaza fm



Imeelezwa kwamba daladala yoyote itakayokatisha root na kutomfikisha abiria katika kituo husika itachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za jeshi la usalama barabarni

Hayo yameelezwa leo na Coplo Martini Richard Mangu wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarni wakati akiongea katika kipindi cha moja kwa moja cha usalama barabarni kinachorushwa na radio na mwangaza fm kila saa moja na nusu hadi saa mbili kamili asubuhi siku za jumatatu hadi ijumaa

Amesmea kuwa  wananchi sasa wapo huru kutoa taarifa moja kwa kwa viongozi wa jeshi la polisi kupitia mitandao ya cm kwa gharama ndogo
Akifafanua jinsi ya kupata namba za viongzi wa jeshi hilo kupitia cm amesema,unaenda sehemu ya msg katika cm yako,unaandika neno polisi Dodoma alafu unatuma kwenda namba 15327

Amesema baada ya kufanya hivyo mtumiaji wa cm atapokea ujumbe mfupi wenye namba za RPC,RCO,OC FFU na RTO wa Mkoa husika,ambapo utakuwa huru kumpatia taarifa yoyote na kupatiwa msaada haraka zaidi
Ufafanuzi huo umekuja baada ya kuulizwa swali na msikilizaji wa radio mwanhaza fm bwana Abel amjiko kulalamika kuwa daladala hasa za zinazokwenda st.Gemma kutowafikisha kituoni hapo

Nae Sanjent Gershom Kitundu wa jeshi la zima moto na uokozi Mkoani dodoma kwa upande wake amesema,stand mpya ya daladala ya jamatini kwa sasa ina wafanyabiashara ambao wapo kisheria wakiihudumia jamii hivyo ni lazima wawe na vifaa maalumu vya kuzimia moto kama sheria inavyoelekeza
neema jua                                                   mwisho 

Post a Comment

AddThis

 
Top