THURSDAY-29-AUGUST-2013
STAND MPYA YA DALA DALA YA JAMATINI MJINI DODOMA
Muonekano wa satand mpya ya daladala ya jamatini na nyakati za usiku kunawaka taa kama mchana
Wananchi na madereva wa daladala Mkoani dodoma wamelalamikia stand mpya ya jamatini kuwa ni ndogo na haikidhi mahitaji
Wananchi hao wameyasema hayo jana baada ya kupata adha ya usafiri na ufinyu wa eneo katika stand hiyo mpya yenye muonekano maridadi
Wamesema eneo la stand ni zuri lakini ni dogo kwani magari ya daladala ni mengi na watu ni wengi hivyo kuruhusu magari ya root zote kusimama katika eneo hilo kwa kushusha na kupakia abiria ni kitendo ambacho wao kama wasafiri na madereva hawakubaliani nacho kwasababu ni mateso
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma bwana Robart Kitimbo amesema ni kweli tatizo hilo lilikwepo kwa kipindi kifupi lakini wamejitahidi kutatua kero hiyo kwa kuruhusu magari mengine kubaki katika stand ya zamani iliyo eneo la oil com karibu na stand ya mabasi yaendayo mikoa mingine yakitokea Dodoma
Magari yaliyoruhusiwa kubaki katika stand ya zamani ni ya root ya nane,area d na swaswa
Lakini pamoja na jitihada hizo bado wananchi wanaona ni kero kwa abiria wengine kushushwa stand nyingine na wengine stand nyingine
SIKILZA HAPA MWANANCHI AKILALAMIKA
Post a Comment