0
WAKATI miamba ya soka nchini, Yanga, Simba, Azam fc na Mtibwa Sugar ikishiriki kombe la Mapinduzi 2015 kisiwani Unguja Zanzibar, maisha ya ligi kuu soka Tanzania bara yanatarajia kuendelea kama kawaida wikiendi hii kwa mechi kadhaa kupigwa.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu, kesho (Januari 3 mwaka huu) Wagosi wa Kaya, Coastal Union watawakaribisha Maafande wa JKT Ruvu katika mechi ya raundi ya 9 ya ligi kuu itakayopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu,  Maafande wa Ruvu Shootings watawaalika ‘Wanankurukumbi’ Kagera Sugar FC kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.
Kagera Sugar waliomfukuzisha kazi kocha wa Simba, Mzambia Patrick Ackson Phiri watakuwa ugenini kwa lengo la kuendeleza dozi yao.
Polisi Morogoro watakabiliana na Stand United katika uwanja wa michezo wa Jamhuri uliopo mjini Morogoro.
Jumapili januari 4 mwaka huu, Nyasi za uwanja wa CCM Sokoine zitawaka moto kwa wenyeji Tanzania Prisons, ‘Wajelajela’ kuchuana na Ndanda fc.
Mechi baina ya Mbeya City fc na Yanga, Azam fc dhidi ya Mtibwa Sugar pamoja na ile ya Mgambo na Simba zimeahirishwa kwani Yanga, Simba, Azam na Mtibwa zipo Zanziba

Post a Comment

AddThis

 
Top