0
Mwanaume mmoja Nigeria amefunguliwa mashtaka baada ya kumfungia mke wake nje ya nyumba yao mpaka asubuhi na kuamua kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 9.
Polisi wamemfungulia mashtaka mwanaume huyo ambaye jina lake ni Osaro mwenye umri wa miaka 55 baada ya kuripotiwa kufanya kosa hilo.
Mama wa mtoto huyo Stella, aliwaambia wachunguzi wa tukio hilo kuwa mumewe alimfungia nje ya nyumba yao saa 2 usiku na yeye kujifungia ndani na mabinti zake wawili.
Siku iliyofuata mtoto huyo alimwambia mama yake kuwa alifanyiwa kitendo hicho na baba yake zaidi ya mara moja, mama huyo akamkagua na kubaini ni kweli alibakwa.
 Binti huyo aliwaeleza Polisi kuwa baba yake ameahi kumfayia kitendo hico zaidi ya mara moja huku mama huyo akisema hiyo si mara ya kwanza kwa mumewe kutenda kosa hilo kwani mara ya kwanza aliwahi kumpa ujauzito mtoto wake wa miaka 17 lakini mama huyo alimsamehe.

Post a Comment

AddThis

 
Top