0
Moja ya historia ya kujivunia ya klabu ya Simba ni kikosi chake kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri mwaka 2003.


Simba iliivua ubingwa Zamalek kwao Cairo, ikaifunga na kuivua taji hilo la Afrika wakati huo ikiwa ni timu bora barani Afrika.

Hiyo ni rekodi, hakuna timu ya Afrika Mashariki imewahi kufanya hivyo.

Aliyepiga penalti ya mwisho baada ya Juma Kaseja kuwa shujaa kupangua penalti za Waarabu hao, alikuwa ni kiungo nyota Christopher Alex Masawe.

Wengi walihoji mchagga kuwa bora kisoka, Masawe alikuwa noma aisee. Sasa mkongwe huyo ni mgonjwa taabani.

Ingawa kumekuwa na taarifa za kuchanganya, wengine wakisema yuko Amana Hospital, Dar wengine wakidai yuko kwao Dodoma.

Ukweli ni kwamba kiungo ni mgonjwa, anahitaji msaada na itakuwa vizuri kumsaidia. Kuanzia wadau wa Simba, wadau wa michezo, kokote alipo, tafadhari jitokezeni mumsaidie huyu mtu tafadhari.

Post a Comment

AddThis

 
Top