Wakati alipokuwa klabuni Simba SC alikataa kufananishwa na aliyekuwa ‘ staa’ wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi kwa madai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa timu Taifa, Taifa Stars alikuwa ba ubora mkubwa kuliko yeye. Namzungumzia, Mbwana Samatta ‘ kipaji cha hali ya juu kutoka Tanzania. Samatta aliichezea Simba kwa miezi minne na kufunga mabao nane katika ligi kuu na mengine matatu katika klabu bingwa Afrika kabla ya kununuliwa kwa dau la dola 100, 000 ( zaidi ya milioni 150) na klabu bingwa mara nne ya kihistoria Afrika, TP Mazembe katikati ya mwaka 2011.
Mfungaji huyo bora wa Kombe la shirikisho Afrika, 2013 kwa sasa yuko katika majaribio na kuna uwezekano mkubwa akasajiliwa na CSKA Moscow ya Urusi. Kama mambo yatanyooka kama tunavyohitaji Watanzania wengi, Samagoal, anaweza kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao. Kitendo tu cha kupata mwaliko kutoka kwa timu hiyo iliyocheza ligi ya mabingwa hatua ya makundi msimu huu ni hatua kubwa lakini hataishia hapo kwa kuwa ni kijana mwenye hitaji kubwa katika soka.
Wakati alipotua TP, Samatta alikutana na changamoto nyingi, lakini kubwa ilikuwa ni kitendo cha mashabiki wengi wa TP kumuweja juu na kumchukulia ‘ mchazaji wao bora klabuni’. Bahati ni kwamba nimekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Samatta kiasi cha kufahamu baadhi ya changamoto anazokutana nazo katika ‘ soka la kulipwa’. Kuna wakati niliwahi kufanya naye mahojiano wakati huo akiwa katika mwaka wake wa kwanza, TP, nilimuuliza mengi lakini kubwa nilihataji kujua kuhusu ‘ ulinganisho wa mashabiki kuhusu yeye na Tressor Mputu.
Kama alivyokataa kulinganishwa na Mgosi, ni hivyo pia Samagoal aliniambia, ‘ Sifanani na Tressor, yeye tayari ana tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika’. Hata kama ndani ya uwanja mashabiki waliona ubora wa Samatta kuliko Mputu, yeye mwenyewe ( samatta) aliendelea kujifunza na kujenga mahusiano mazuri zaidi ya ndani na nje ya uwanja na Tressor huku akichukulia kitendo cha kucheza timu moja na mchezaji huyo bora wa Afrika, 2009
Wakati akitua TP, timu hiyo ilikuwa na washambuliaji, Tressor na Given Singuluma lakini juhudi binafsi ikiwemo kukubali kucheza nje ya nafasi aliyoizoea kulimfanya Samatta kupata nafasi kikosi cha kwanza huku mabao yake sita katika ligi ya mabingwa Afrika, 2012 yakimpatia nafasi ya kupangwa sambamba na Tressor katika safu ya mashambulizi na Mzambia, Singuluma akawa akicheza eneo la kiungo. Samatta alipenya taratibu katika kikosi cha kwanza, TP lakini bado alikuwa na ‘ usongo’ uleule. Upi huo?.
Miaka minne iliyopita alisema, TP ni njia tu, kituo kipo Ulaya. ; “ Kwa kweli nakosa mpaka maneno ya kumuelezea, ila nabaki kuamini kuwa Mungu ana baraka zake. Sijapata kufikiria kama kipaji kile ni mdogo wangu wa kuzaliwa tumbo moja, katika vipaji ambavyo vipo duniani Mbwana ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na namuweka katika orodha ya wachezaji 20 bora wenye vipaji vikubwa duniani. Kwa sababu ni Mtanzania anaweza kuonekana ni mchezaji wa kawaida, lakini kile ni kipaji maridhawa ambacho nimewahi kukiona. Ndiye mchezaji ambaye namkubali sana nchini. Ni kipaji ambacho ametunikiwa na Mungu. Nina imani atakuwa mbali sana akicheza mpira wa kulipwa ulaya,au la basi anaweza kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Africa kama ataongeza mkataba pale TP Mazembe” anasema Mohamed Samatta mchezaji wa JKT Mgambo na kaka wa Mbwana.
Hata kabla ya ofa ya CSKA, Samatta amekuwa mtulivu, mvumilivu, na kmiakkiwa na kijana msikivu mwenye ndoto kubwa. Amefanikiwa kwa kiasi chake na wakati huu umri wa miaka 21, Ulaya ni kituo muhimu alichopanga kufika. Hana makuu licha ya kuwa staa wa kweli katika soka la DRC, Afrika na kitendo cha kuwaheshimu wachezaji kama Mgosi na Tressor wakati akitengeneza jina kimechangia mafanikio hayo sasa kuna nafasi kubwa ya Mtanzania huyo kucheza sambamba na Zoran Tosic, mshambulizi wa Serbia ambaye Sir Alex Ferguson alitoa pauni 17 milion na kumpeleka Manchester United katikati ya mwaka 2008.
Labda inaweza kutokea siku Mbwana Samatta akacheza ligi ya mabingwa ulaya, kwani CSKA Moscow ni timu ya mara nyinfi katika michuano hiyo na msimu huu wameondolewa katika hatua ya makundi baada ya kumaliza nyuma ya FC Bayern Munich, Manchester City na AS Roma. Inaweza kuwa ndoto ya kweli, ni jambo la kusubiri na kuona kabla ya ili kuona kama kweli, Samagoal ataingia tena katika ushindani wa namba na Zoran, baada ya kufanikiwa dhidi ya Mgosi na Tressor huku akiwapa heshima kubwa.
“ Nachoweza kusema nimekuwa makini na mtulivu, na wakati mwingine huwa nasema ni bahati kutoka kwa Mungu. Mimi ni ‘ mwanajeshi wa mbele’ mshambulizi wa kwanza kabisa, hivyo ndivyo ninavyotumika katika klabu yangu na nimekuwa nifunga mabao ya kutosha kutokana na kupangwa katika nafasi hiyo nayoipenda. Mchezaji huwezi kujichagulia nafasi ya kucheza katika timu, mahitaji ya Mwalimu ndiyo jambo la msingi. Napenda kucheza katika nafasi yoyote nayopangwa kutokana na mfumo wa kocha anavyotaka” anasema Samatta
Post a Comment