0
Watoto huwa hawajui kuficha hisia, kama akipenda huonyesha anapenda kweli na kama anachukia kitu pia hawezi kuficha kama anachukia.
Mtoto mmoja alionyesha kuvutiwa na Justin Timberlake alipokuwa akiperform kwenye stage ya  Barclays Center, Marekani Jumapili December 14  ambapo mtoto mmoja liyekuwa amevaa suti na tai yake safi alikuwa na zawadi ya Justin mkononi na alipoonyesha ishara ya kumtaka msanii huyo apokee zawadi yake, jamaa alisimamisha show na kuipokea.
Zawadi hiyo ilikuwa imefungwa poa kabisa, alipofungua alikuta zawadi aliyopewa ilikuwa ni tai, Justin alifurahishwa sana na zawadi hiyo.
… Una miaka kumi, umekuwa ukiniangalia tangu una miaka miwili… Hey man, hii ni zawadi kubwa sana… Kwa sababu gentleman hawezi kuvaa tai mbili, hii nitaivaa siku ya Christmas… Nakupenda…“– Justin Timberlake.
Justin alijikuta akishindwa kujizuia kutokwa machozi baada ya kusema hayo.
Unaweza kuitazama video ya tukio hilo hapa.

Post a Comment

AddThis

 
Top