0
Staa ambaye huenda anaongoza kutokea kwenye headlines nyingi zaidi za vyombo vya habari vya Kimataifa akiwakilisha 254, Lupita Nyong’o ameendelea kung’aa na kwa hii ya leo ni ishara tosha kwamba 2014 ulikuwa wa neema kwake na bado 2015 una dalili zote za neema kendelea kumshukia staa huyo.

12 Years a Slave‘ ilimfungulia njia nzuri ya Dunia yote kumfahamu, baada ya hapo deal kibao zimemuangukia ikiwa ni pamoja na za uanamitindo ambapo ameshakusanya tuzo kadhaa ikiwemo ile ya mwanamke mzuri zaidi duniani na tuzo ya Oscar.

Deal mpya ni kwamba anatarajia kuingia location muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kushoot movie mpya ya ‘Americanah’ ambayo atakuwa staa akishirikiana na David Oyelowo  ambapo movie hiyo ni story iliyotokana na novel ya ‘Chimamanda Ngozi Adichie’ kilichoandikwa Nigeria.

Kampuni ya Brad Pitt ambayo ilitayarisha pia movie ya 12 Years a Slave inahusika kuitayarisha hii pia, hakika baada ya zile Oscar na Grammy award alizonazo mkononi kuna nyingine tuzitarajie, 2015 bado ni mwaka wake aisee.

Post a Comment

AddThis

 
Top